Bobi avunja rekodi ya kuwa mbwa mwenye umri mrefu Zaidi duniani

Bobi avunja rekodi ya kuwa mbwa mwenye umri mrefu Zaidi duniani

Mbwa mwenye umri wa miaka 30 nchini Ureno  ametajwa kuwa ndiye mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kutokea duniani, shirika la Guinness World Records limeeleza.

Bobi ambae ni aina safi ya Rafeiro do Alentejo yenye wastani wa kuishi miaka 12 hadi 14.

Habari hizi zimekuja wiki mbili tu baada ya Spike the Chihuahua mwenye umri wa miaki 23, kupewa rekodi ya mbwa mwenye miaka mingi Zaidi .

Mbwa wa zamani zaidi kuwahi kutokea alikuwa Bluey wa Australia, ambaye alikufa mnamo 1939 akiwa na umri wa miaka 29 na miezi mitano. Kwa upande wa Bobi  1 Februari alikuwa na umri wa miaka 30 na siku 226.

Hili limethibitishwa na hifadhidata ya wanyama kipenzi ya serikali ya Ureno, ambayo inasimamiwa na Muungano wa Kitaifa wa Madaktari wa Mifugo, kulingana na Guinness World Records.

Bobi ameishi maisha yake yote na familia ya Costa katika kijiji cha Conqueiros, karibu na pwani ya magharibi ya Ureno, baada ya kuzaliwa na ndugu watatu katika jengo la nje.

Leonel Costa, ambaye alikuwa na umri wa miaka minane wakati huo, alisema wazazi wake walikuwa na wanyama wengi na ilimbidi kuwaweka chini watoto hao, lakini Bobi alitoroka.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post