Mwenyekiti wa Bodi ya Sauti za Busara, Simai Mohammed Said, leo Februari 15, 2025 amefungua siku ya pili ya tamasha hilo katika viwanja vya Mji Mkongwe, Stone Town kisiwani Unguja.
Mwenyekiti huyo amefungua kwa wimbo uitwao Afrika wa kwake Salif Keita (Mali) . Wimbo huo uliotoka mwaka 1995 unaendelea kuishi katika historia ya muziki Afrika kutokana na maudhui yake ya upendo, umoja, na kujivunia urithi wa bara la Afrika.
Katika wimbo huo, Salif anahimiza umoja miongoni mwa Waafrika na kuutangaza utamaduni wa bara la Afrika ulimwengu. Anasisitiza kuwa, licha ya changamoto nyingi zinazokumba bara hili, Afrika inastahili kujivunia na kupigania haki zake.
Salif Keita alizaliwa mwaka 1949 nchini Mali wengi wanamfahamu kutoka na sauti yake ya kipekee akiimba muziki wa asili wa Mali, Jazz, Blues, na Pop.
Keita, ambaye ni miongoni mwa wanamuziki wa kwanza kutoka Afrika Magharibi kuleta mapinduzi katika muziki wa kimataifa, ana Albam zaidi ya kumi kati ya hizo ni Moffou (2002), Amen (1991), Soro (1987) na Un Autre Blanc (2018).
TAZAMA VIDEO HIYO KUPITIA INSTAGRAM YA @Mwananchiscoop

Leave a Reply