Utafiti: Brazili Yashika Namba Moja Nchi Inayopenda Kuoga

Utafiti: Brazili Yashika Namba Moja Nchi Inayopenda Kuoga

Kulingana na utafiti uliyofanywa na kampuni ya ‘Kantar Worldpanel’, unaeleza kuwa nchi ya Brazil inashika nambari moja kama nchi inayopenda kuoga zaidi duniani, ikiwa na wastani wa kuoga mara 14 -16 kwa wiki.

Utafiti huo unaeleza kuwa Wabrazil wanazingatia sana usafi wa mwili kutokana na hali ya hewa ya nchi hiyo ambayo inakadiriwa kuwa na joto la wastani wa 24.6°C ikiwa ni tofauti na nchi nyingine kama Uingereza yenye wastani wa joto 9.3°C.

Mbali na hilo lakini pia watafiti hao wanabaini kwamba zipo nchi ambazo zinatofautiana katika muda wa kuoga ambapo Wabrazi wanatumia mpaka dakika 10 kwa ajili ya kuoga huku Wamarekani wakitumia dakika 9 na Waingereza dakika 9.6






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags