Ulaji Tambi Mara Kwa Mara Unachochea Magonjwa Haya

Ulaji Tambi Mara Kwa Mara Unachochea Magonjwa Haya

Kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa na ‘Chuo Kikuu cha Baylor’ umeeleza kuwa ulaji wa tambi mara kwa mara haswa mara mbili hadi tatu kwa wiki, umehusishwa na hatari kubwa ya matatizo ya afya kama magonjwa ya moyo, kiharusi, na kisukari.

Utafiti huo uligundua matatizo hayo ya kiafya kwa watu waliokula chakula hicho mara nyingi zaidi na kuonesha kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata ‘Metabolic Syndrome’, mkusanyiko wa hali zinazoongeza hatari ya magonjwa hayo.

Mbali na hilo lakini pia watu ambao walionesha kuwa hatarini zaidi ni wanawake huku wataalamu wa afya wakipendekeza watu kuacha kula tambi mara kwa mara na kuanza kula chakula bora na vya asili ili kupunguza hatari hizo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags