Rapa wa Marekani Rick Ross ameonesha nia ya kununua mjengo wa msanii Cardi B baada ya rapa huyo kudai kuwa ameuchoka.
Kupitia kwenye mtandao wa X zamani Twitter Rapa huyo wakike Cardi B alishare picha ya mjengo huo huku akiandika kuwa “My Casa I don’t want it nomore tho” akiwa na maana Nyumba yangu lakini nimeichoka siitaki tena.
Baada ya kutoka kauli hiyo Rapa Ross anayetamba na nyimbo kama ‘Champagne Moments’ alikomenti kwa kumtaka msanii huyo aseme bei ya mjengo huo.
Utakumbuka kuwa Cardi alikuwa akiishi kwenye mjengo huo na aliyekuwa mumewe Offset ambapo baada ya wawili hao kutengana Offset alihama kwenye nyumba hiyo na kumuacha Cardi peke yake.
Leave a Reply