Rapa kutoka Marekani Offset amewasilisha madai mahakamani akitaka kushiriki malezi ya pamoja ya watoto wao na aliyowapata na aliyekuwa mke wake Cardi B.
Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama zilizowasilishwa Jana Ijumaa, Februari 28, Offset anataka haki sawa yeye na Cardi B katika malezi ya watoto wao.
Mbali na kutaka kushiriki malezi pamoja lakini pia Offset ameomba usawa katika mgawanyo wa mali ambazo wamezichuma pamoja kwenye ndoa yao huku akitaka kila mmoja kutumia gharama zake binafsi kuwalipa wanasheria katika kesi hiyo.
Ikumbukwe wawili hao wamekuwa kwenye migogoro kwa muda mrefu huku wakitengana rasmi mwaka jana 2024 ambapo sababu kubwa ya kuachana kwako Cardi alidai kuwa mzazi mwenzie huyo alikuwa akifanya usaliti mara kwa mara.
Cardi B na Offset wana watoto watatu pamoja ambao ni Kulture Kiari Cephus, Wave Set Cephus, na Binti wa tatu aliyezaliwa Septemba 7, 2024 huku jina lake likiwa halijafahamika mpaka kufikia sasa.

Leave a Reply