Namna ya kupika tambi za nazi

Namna ya kupika tambi za nazi

Ramadhani Kareem! Kama tunavyojua mwezi huu ni mwezi wa kula vitu laini laini. Basi Mwananchi Scoop hatuwezi kukaa kimya tupo na wewe sako kwa bako kuhakikisha unapata cha kufungulia kinywa katika mfungo huu wa Ramadhani. 

Ikiwa ndiyo tupo kumi la kwanza tumekusogezea kitu chepesi kabisa ambacho unaweza kukiweka katika ratiba yako ya futari. Namna ya kutengeneza Tambi za Nazi. 

MAHITAJI

  • Tambi (spaghetti 1-2) inategemea na wingi wa watu
  • Nazi kubwa mbili zilizosagwa tayari
  • Sukari kiasi
  • Hiriki, pilipili mtama kijiko kidogo
  • Dhabibu kavu kiasi
  • Chumvi kiasi

JINSI YA KUANDAA

  • Chukua nazi yako na uichuje tui zito kabisa na kisha uiweke pembeni
  • Baada ya hapo chuku tambi zako na uanze kuzikata size unayopenda, ukishamaliza bandika sufuria ya maji jikoni weka chumvi kiasi na uache mpaka pale maji yatakapopata moto.
  • Maji yakishapata moto weka tambi zako na uache zichemke kiasi, kisha zitoe na uzichuje
  • Ukishamaliza hapo chukua sufuria nyingine weka tambi zako, weka hiriki, pilipili mtama kiasi pamoja na tui la nazi
  • Baada ya hapo injika jikoni na ukoroge tui lako lisiweze kukatika, likishakaa sawa acha tambi zako ziive kwa moto mdogo kabisa.
  • Tui lako likishakauka chukua dhabibu weka juu kisha zifunikie kama unavyofunikia wali (unazipalilia na makaa juu) na kwa wale ambao wanatumia Oven basi wataziweka kwenye ovena mpaka pale zitakapo kauka vizuri.

Mpaka kufikia hapo tambi zako zitakuwa tayari, unaweza kula kwa mchuzi wa nyama, maini, maziwa, chai na hata juice. Kwa wale wanaouza futari siyo kila siku uwapikie wateja za mafuta siku moja moja badilisha ili kuwavutia zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags