Mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Muhozi Kainerugaba amezua gumzo mtandaoni baada ya kuonesha kuvutiwa na mwanamuziki kutokea Nigeria Ayra Starr.
Kupitia mtandao wake wa X Disemba 29, 2024 Muhoozi aliandika kuwa amepewa ruhusa na babu yake anaefahamika kama mzee Amos ya kutafuta mwanamke yeyote Duniani huku akionesha kuvutiwa na Ayra Starr zaidi.
"Marehemu Babu yangu...Mzee Amos alinipa ruhusa ya kupata mwanamke yoyote Duniani nitampata Ayra Starr" ameandika Muhoozi.
Hata hivyo kauli hiyo imepokelewa na mitazamo tofauti tofauti na watumiaji wa mitandao wapo waliona kama utani na masihara wengine wakihusisha matumizi ya mitandao ya kijamii na siasa, Lakini kwa upande wa Ayra Starr hajatoa maoni yoyote juu ya kauli ya Muhoozi.
Jenerali Muhoozi Kainerugaba ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda CDF kwenye Jeshi la Ulinzi la Watu wa Uganda UPDF. Aliteuliwa kushika wadhifa huu na baba yake Rais Yoweri Kaguta Museveni tarehe 21 Machi, 2024.
Leave a Reply