Mtoto wa Michael Jordan, Marcus Jordan anatuhumiwa kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Cocaine pamoja na kuendasha gari akiwa amelewa.
Marcus mwenye umri wa miaka 34, alikamatwa na kufungiwa katika gereza la Orange, Florida Marekani leo Februari 4, 2025 kulingana na rekodi za jela.
Hata hivyo Marcus aliachiwa huru baada ya kuwekewa dhamana ya dola 4,000 kwa ajili ya kuachiliwa kwake.
Utakumbuka kuwa hivi karibuni Marcus alionekana akila bata na mke wa zamani wa Eddie Murphy mwanamitindo Nicole Murphy, mwenye umri wa miaka 56.
Ambapo wawili hao walionekana wakiwa kwenye tamasha la DJ Khaled 'We the Best Foundation x Jordan Golf Classic' mjini Miami.
Leave a Reply