Katika ulimwengu wa muziki na sanaa, uwezo wa msanii kufanya utumbuizaji wa moja kwa moja 'live performance' ni mojawapo ya vipengele muhimu zaidi vinavyochangia mafanikio na ufanisi wake. Live performance humwezesha msanii kupata nafasi ya kuwasiliana na mashabiki wake ana kwa ana. Kuonyesha kipaji chake na kujenga uhusiano wa kipekee na watazamaji.
Kawaida live performance inampa msanii nafasi ya kuonyesha uwezo wake halisi. Kwani inakuwa tofauti na muziki ambao unarekodiwa studio na kupita katika mchujo wa sauti.
Hata hivyo live performance inatoa fursa ya kipekee kwa msanii kuungana na mashabiki wake. Wakati wa kutumbuiza, msanii anaweza kuona mwitikio wa moja kwa moja kutoka kwa watazamaji kama vile vibe la kutosha.
Hii inamfanya msanii kujua ni wimbo gani unawagusa zaidi mashabiki na pia inawasaidia mashabiki kujisikia kuwa sehemu ya msanii, jambo ambalo.
Katika hilo maonyesho ya moja kwa moja yakifanywa vizuri ni njia ya kujitangaza na kukuza umaarufu kwa msanii na kujizolea mashabiki wapya.
Pia katika live perfomance ni rahisi msanii kubadilisha au kuongeza mbwembwe na vionjo kwenye nyimbo zake. Hii humpa nafasi ya kuonekana ubora wake zaidi kwa mashabiki.
Aidha ni njia nzuri na rahisi kwa msanii katika upande wa biashara. Inaweza kumpa fursa ya kuuza tiketi, bidhaa (kama vile t-shirt, CD, na vifaa vingine). Lakini pia onyesho linaweza kufungua milango ya mikataba ya kibiashara kama vile udhamini.
Licha ya kuwa wapo wasanii maarufu na wanaofanya vizuri Bongo. Lakini bila kuwa na uwezo wa kufanya live perfomance wanahesabika kama siyo wasanii kamili .
Akizungumza na Mwananchi msanii wa muziki wa Hip-hop Christian Bella ambaye amekuwa akilitumikia jukwaa mara nyingi kwa live perfomance amesema hicho ndicho kigezo cha kumpima msanii kama amekamilika.
"Yaani msanii bila kujua 'live perfomance' sidhani kama wewe tunaweza kukuhesabu kama umekamilika. Hapo utakuwa bado haujakamilika, 'live pefomance' ndiyo ubora wa msanii kwa kuweza kufanya hivyo ndiyo inaonesha wewe umekamilika," amesema Bella.
Aidha kwa upande wa mwanamuziki na prodyuza Baba Khash amesema muziki unaosikilizwa na mashabiki unapitia njia nyingi za mchujo hivyo ubora wa msanii ni katika utumbuizaji wa moja kwa moja.
"Live perfomance kwa msanii ni muhimu sana kwa sababu ukiona hajiwezi kufanya hivyo ujue siyo muimbaji. Mimi pia ni prodyuza naona wasanii tunavyosumbuana studio. Unakuta mtu anarudia sana hadi kupata kitu kizuri.
"Mashabiki hawajui wanakuja tu kusikia muziki umenyooka, tena wengine maarufu sana lakini bila kufahamu ilikuwa shida wakati wa kurekodi yani msanii unakuta karudia sana," amesema.

Leave a Reply