Maneno ya Nduttu Baada Ya Kukosa Tuzo TCA

Maneno ya Nduttu Baada Ya Kukosa Tuzo TCA

Mchekeshaji Nduttu ni mmoja kati ya waliokuwa wakiwania tuzo za ucheshi kupitia kipengele cha 'Best Upcoming Stand up Comedian of the year'. Kwenye tuzo za Tanzania Comedy Award zilizofanyika usiku wa kuamkia leo ukumbi wa The Super Dome Masaki, mgeni rasmi akiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Nduttu ambaye bahati haikuwa upande wake, hakufanikiwa kunyakua tuzo hiyo, Akizungumza na Mwananchi Digital usiku wa kuamkia leo baada ya washindi wa vipengele vyote kutangazwa amesema kila aliyeshiriki kwenye tuzo hizo anastahili hongera haijalishi ameshinda au hajashinda.

"Mimi napenda iwe ni hongera kwa kila mtu aliyeshiriki kwenye tuzo hizi. Kwasababu ilikuwa ni ushindani na kila mtu ameonesha kipaji chake kwa nafasi yake. Lakini mwisho wa siku anayeruhusu nani apate na nani asipate ni Mungu. Yaani kama mtu aliyefaulu na anasubiria kupangiwa shule kwahiyo usipopangiwa haimaanishi hauna akili.

"Kwahiyo ni hongera kwa kila mchekeshaji kwa kuwa tasnia sasa imekuwa kwa mara ya kwanza ni watu wengi walikuwa wanachukulia vituko. Lakini kama tumekuwa na Rais Samia ni kitu kikubwa sana kwetu na kitu sahihi kuwa na tuzo zetu za comedy. Mwanzoni tulikuwa tunaingia kweye tuzo za filamu kwa kuchomekeana sasa rasmi tuna tuzo zetu kama umekosa mwaka huu inakuwa chachu ya kufanya kazi," amesema Nduttu.

Hata hivyo, Nduttu ametoa tathmini yake kwenye tuzo hizo ambazo zinafanyika kwa mara ya kwanza na kusema hakuna upendeleo wowote uliofanyika kwa sababu kila mtu aliyeshinda tuzo hizo alistahili.

"Hakuna upendeleo wowote kwangu. Kwa sababu kila aliyepata alistahili na hata ulikuwa ukiangalia vipengele vya tuzo vyote ukiambiwa tuchagulie mchekeshaji atakayeshinda humuoni. Yaani ukimgusa Leonardo noma, Steve Mweusi noma, ukimgusa Jol Master noma kwahiyo mwisho wa siku ni nafasi ambayo Mungu amempa mtu ndiyo inakuja kuamua hivyo," amesema






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags