Janet Jackson Atunukiwa Tuzo Ya Heshima

Janet Jackson Atunukiwa Tuzo Ya Heshima

Mwanamuziki na Muigizaji kutoka nchini Marekani, Janet Jackson usiku wakuamkia leo Mei 27, 2025, ametunukiwa tuzo ya heshima ‘Icon Award’ katika hafla ya utoaji wa tuzo za ‘American Music Awards’.

Wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Jumatatu usiku, nyota huyo alitumbuiza baadhi ya nyimbo zake bora zaidi, ikiwa ni pamoja na Someone to Call My Lover na All for You. Hatahivyo tamasha hilo lilishuhudia uigizaji wake wa kwanza wa moja kwa moja katika TV tangu 2018.

“Mimi kila siku kuheshimiwa tuu, ninashukuru sana. namaanisha hakuna dharau kwa njia yoyote nimewahi kutana nayo, lakini pia sikufikiria mwenyewe kama ningetunukiwa tuzo ya icon." amesema Janet.

Janet ambaye kwa sasa anaumri wa miaka 56, aliendelea kutafakari mwanzo wake katika tasnia ya muziki akitokea katika familia ya muziki ya mzee Jackson na dada mdogo wa marehemu Michael Jackson.

"Familia yangu, mimi mwenyewe, ndoto yetu haikuwahi kuwa maarufu. Hatukulelewa hivyo. Daima tulikuwa na upendo maalum kwa muziki, kucheza, kuimba, Umaarufu ulikuja na matokeo ya kufanya kazi kwa bidii na kujitolea. Hadithi yangu, hadithi ya familia yangu kwa kweli ni hadithi ya Marekani. Hili lingetokea Amerika pekee." amesema Janet.

Kwa kumalizia, Janet alisema kuwa anatumaini ushindi wake utakuwa na msukumo kwa wasanii wengine na pia aliishukuru timu yake na mashabiki kwa sapoti wanayoendelea kumpatia.

"Kwa sababu yako na Mungu, nimesimama hapa, Nataka kuwashukuru AMAs kwa heshima hii, ambayo ninashukuru kwa unyenyekevu na mwisho kabisa, nataka kusema muweke Mungu katika kila sehemu ya maisha yenu kwa sababu huko ndiko anakotaka kuwa. Ninawapenda sana." amesema Janet.

Wasanii wengine ambao wamewahi kutunukiwa tuzo hiyo ya heshima katika tuzo za American Music Awards ni pamoja na Rihanna na Lionel Richie.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags