Aliyemshtaki Jay-Z Adai Kushinikizwa Na Wakili

Aliyemshtaki Jay-Z Adai Kushinikizwa Na Wakili

Baada ya rapa Jay Z kufutiwa kesi iliyokuwa ikimkabili na Diddy wakishtumiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 13 mwaka 2000 kwenye tuzo za video za muziki MTV Award, Mwanamke huyo amerudi tena na kukanusha madai hayo.

Katika mahojiano yaliyovuja na kuchapishwa na ABC News, mwanamke huyo amekanusha madai hayo akisema kuwa Jay Z hakumbaka akidai wakili wake Tony Buzbee ndiye alimshinikiza kuwasilisha kesi hiyo dhidi ya rapa huyo.

Hata hivyo, rapa Jay-Z amefungua kesi ya kashfa dhidi ya mwanamke huyo na wakili wake Tony Buzbee, akiwashutumu kwa njama ya kumchafua jina na kumdhalilisha.

Utakumbuka, Kesi ya awali ambayo iliwasilishwa na mwanamke huyo ambaye jina lake halikuwekwa wazi, Oktoba 20, 2024, akidai kuwa Sean "Diddy" Combs alimnyanyasa kingono msichana huyo kwenye sherehe baada ya Tuzo za Muziki za MTV mwaka 2000 akiwa na miaka 13.

Katika malalamiko yaliyorekebishwa, yaliyowasilishwa Desemba 2024, 'Jay Z' aliongezwa kama mshtakiwa na akashutumiwa kwa ubakaji. Hata Hivyo Jay Z, alikanusha vikali madai hayo, huku akimtaka mlalamikaji 'Doe' kufungua kesi ya jinai na siyo ya madai kama alivyofanya endapo anaamini madai yake yana ukweli wowote dhidi yake.

Mapema mwaka huu mawakili wa mwanamke huyo walitoa taarifa ya mteja wao kufuta kesi dhidi ya Jay-Z na Diddy huku uamuzi huo ukiwa na kipengele cha kutofunguliwa tena kesi hiyo katika siku za mbele kwakuwa madai hayo hayakuwa na ukweli wowote uliyo thibitishwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags