Mahakama inayoendesha kesi ya mauaji ya Rapa Pop Smoke imemuhukumu miaka 29 jela Corey Walker, mwenye umri wa miaka 24 ambaye ni mmoja wa washtakiwa wa mauaji ya rapa huyo wa Brooklyn yaliyofanyika 2020 jijini Los Angeles, Marekani.
Mnamo Februari 4,2025 Walker alikiri makosa ya kuua bila kukusudia na wizi baada ya kuvamia nyumba na kupora. Tukio lililosababisha kifo cha rapa huyo.
Walker, ambaye alikuwa na umri wa miaka 19 wakati wa mauaji hayo ndiye alikuwa mtu mzima pekee kati ya watu wanne waliokamatwa kwa kumuua Pop Smoke. Washtakiwa wengine watatu kesi yao inaendela katika mahakama ya watoto ambapo mnamo Mei 2023, mshukiwa mwingine wa kesi hiyo alikiri kuwa na hatia ya mauaji katika mahakama ya watoto.
Wakati huo huo, mshtakiwa mwingine, ambaye alikuwa na umri wa miaka 17 wakati wa tukio hilo, alikiri makosa ya mauaji na wizi katika mahakama ya watoto ya Inglewood mnamo Aprili 2023 mbapo alipokea kifungo cha miaka minne na miezi miwili.
Leave a Reply