African Giant albamu kutoka kwa Burna Boy bado inasumbua kwenye kiwanda cha muziki Afrika baada ya kuweka rekodi mpya ya kuwa album ambayo imesikilizwa zaidi kwenye kwenye mtandao wa Spotify.
Album hiyo ambayo iliachiwa rasmi Julai 25, 2019 ikiwa ni albamu ya 4 ya msanii huyo imefanikiwa kusikilizwa zaidi ya mara Billion 1 Spotify na kukaa kileleni kama albamu namba 1 Afrika kuanzia miaka ya 2010 kufikia kiwango hicho cha wasikilizaji.
Album hiyo ina jumla ya ngoma 19 ambazo zilifanya vizuri ikiwemo Gbona, Different, Pull Up, Omo, Dangote na nyingine nyingi.
African Giant ilishinda albamu Bora ya Mwaka katika tuzo za All Africa Music Awards za 2019 na iliteuliwa kuwania kipengele cha albamu bora za Muziki ulimwenguni katika Tuzo za 62 za Grammy.
Leave a Reply