Mwalimu Nkya kutoka shule ya msingi Miririni mkoani Arusha alimpa adhabu mwanafunzi Milcah Zakaria Mbise mwenye umri wa miaka 11 wa darasa la 4 ambayo ilimuumiza mkono.
Tangu novemba 2022 binti huyo amekuwa akiteseka kwa kutumia mkono wa kushoto kuandika shuleni, akizungumza na moja ya chombo cha habari mama wa Milcah amesema.
“siku ya tukio mtoto alirudishwa akiwa hajitambui, akatibiwa lakini mkono wa kulia hauna nguvu, nilishtaki kwa mwenyekiti wa kijiji naye akaniambia mwanaye pia alichapwa hadi akaharisha damu”alisema mama huyo.
Na alipokwenda shuleni anaposoma binti huyo kuwaambia walimu kwa kitendo walicho kifanya kwa binti yake lakini wakalazimisha huyo mwanafunzi asome hivyo hivyo huku akitumia mkono wa kushoto kuandikia.
Hakukua na hatua yoyote dhidi ya walimu au yule mwalimu alie sababisha mkono wa huyo binti kupooza hakuonyesha msaada wowote.
Leave a Reply