Billie Eilish: Sijawahi kuumizwa kwenye mapenzi

Billie Eilish: Sijawahi kuumizwa kwenye mapenzi

Mwanamuziki wa Marekani Billie Eilish ameweka wazi kuwa hajawahi kuachwa wala kuumizwa kwenye mapenzi, badala yeye ndiye huwa wa kwanza kutaka kuachana.

Eilish ameyasema hayo wakati alipokluwa kwenye mahojiano na ‘Lana Del Rey’ siku ya jana Alhamis Mei 13, 2024 kwa kueleza kuwa yeye huwa ni mtu wa kuvunja moyo pindi unapokuwa kwenye mahusiano naye na ndio maana huwa hajawahi kuumizwa na mapenzi.

“Sitazungumza kwa undani zaidi, kwa sababu nitakuwa mkorofi, mimi ni mtu wa kuvunja moyo, mkali, mkatili na ndiyo maana sijawahi kuachwa.Na pia, sijawahi kuumizwa mimi huwa ndiyo naacha.” alisema

Mshindi huyo wa Grammy mara tisa amewahi kuhusishwa kutoka kimapenzi na waigizaji Brandon Quentin Adams na Matthew Tyler Vorce pamoja na mwanamuziki Jesse Rutherford ambaye alitemana naye Mei 2023, lakini sasa anahusishwa kutoka kimapenzi na Quenlin Blackwell.

Billie Eilish (22) anatamba na ngoma zake kama ‘Everything i wanted’, ‘Lovely’, ‘No Time To Die’ na nyinginezo huku wimbo uliyomfanya akusanye tuzo zaidi mwaka 2023 ukiwa ni wa ‘What Was I Made For?’ uliyotumika katika filamu ya ‘Barbie’ iliyoachiwa Julai 2023.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags