Bilionea Larry atangaza kwenda kushuhudia mabaki ya Titanic

Bilionea Larry atangaza kwenda kushuhudia mabaki ya Titanic

Licha ya watu watano kufariki na meli ya #OceanGate mwaka jana, bilionea kutoka jimbo la #Ohio nchini #Marekani Larry Connor ametangaza kuwa ana mpango wa kuanza safari ya kuelekea kwenye mabaki ya meli ya #Titanic.

#Connor ameweka wazi kuwa amepanga safari hiyo kwa ajili ya kurudisha heshima katika sekta hiyo, ambapo atashirikiana na watengeneza meli za #Triton ili kuunda chombo cha hali ya juu, cha watu wawili kinachoweza kustahimili shinikizo kubwa linalopatikana kwenye kina cha eneo la ajali ya Titanic.

Aidha kwa mujibu wa vyomba vya habari nchini humo, inasemekana mmiliki wa meli za Triton, Lahey alitengeneza meli yenye thamani ya dola milioni 20 iitwayo ‘Triton 4000/2 Abyssal Explorer’, ambayo #Connor anaamini inaweza kustahimili safari yake kuelekea kwenye mabaki ya meli ya #Titanic.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags