Biles awatolea povu wanaokosoa nywele zake

Biles awatolea povu wanaokosoa nywele zake

Mtaalamu wa mazoezi ya viungo kutoka Marekani Simone Biles amewatolea povu baadhi ya mashabiki waliokuwa wakikosoa mtindo wa nywele zake kwenye mashindano ya Olimpiki 2024.

Kupitia Instagram yake Biles alifunguka kwa kudai kuwa wakati anakwenda katika shindano hilo nywele zake zilikuwa vizuri lakini alipokuwa kwenye Basi alianguka na kusababisha nywele kuvurugika.

Mshindi huyo wa medali tano za dhahabu katika michezo iliyofanyika katika majira ya joto aliwataka wanaohangaika kukosoa nywele zake wampumzishe kwani anampango wa kushughulika na wote watakaonyanyua mdomo kukosoa nywele hizo.

Hii si mara ya kwanza kwa Biles kujitetea kuhusiana na nywele zake kwani katika filamu yake ya ‘Simone Biles: Rising SB’ alijitetea kwa kudai kuwa ulikuwa ni uzembe wa timu yake kwa kutokuwa na mwonekano wa nywele mbaya.

Licha ya mwanadada huyo kukosolewa na mashabiki lakini ukosoaji huo haukumfanya Biles kutoka nje ya mchezo kwani yeye na wenzake wa Timu ya USA walitwaa medali za dhahabu wakati wa fainali ya Gymnastics.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags