Bifu la Quavo na Chris Brown lapamba moto

Bifu la Quavo na Chris Brown lapamba moto

Baada ya ‘rapa’ Quavo kumjibu mwanamuziki Chris Barown kupitia ngoma yake ya ‘Tender’ ambayo mashairi yake yanamtuhumu Brown kuwa alikuwa akimdhalilisha mpenzi wake wa zamani, na sasa Chris amemjibu Quavo kupitia ngoma yake ya ‘Weakest Link’.

Kupitia ngoma hiyo Chris amemchana Quavo kupitia mashairi yake yaliyokuwa yakieleza kuwa ulilala na ex wangu lakini hata mimi pia nililala na ex wako wakati bado upo naye, na kwa mujibu wa baadhi ya vyombo vya habari vinadai kuwa ex wa Quavo aliyelala na Brown ni Saweetie.

Quavo na Chris Brown wapo katika bifu toka mwaka 2017 baada ya #Quavo kudaiwa kutoka kimapenzi na aliyekuwa mpenzi wa #ChrisBrown Karrueche Tran.

Aidha wasanii wa hip-hop nchini Marekani wapo moto kurushiana madongo kupitia ngoma wanazoziachia ambapo siku mbili zilizopita mwanamuziki Drake ameposti ngoma yake mpya ambayo ametumia AI kuingiza sauti ya Snoop Dogg na Marehemu Tupac ngoma hiyo ikidaiwa kuwa amemjibu Kendrick Lamar huku Drake akimtaka Lamar kujibu ngoma hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags