Bien akoshwa na Wivu ya Jay Combat
Mwanamuziki kutoka Kenya, Bien Baraza anayetamba na wimbo wa ‘Extra Pressure’ aliyoshirikishwa na Bensoul amekoshwa na singeli ya ‘Wivu’ inayotamba katika mitandao ya kusikiliza na kuuza muziki nchini huku akiwataka wasanii wa Bongo kujikita zaidi kwenye singeli.
Bien ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye mahojiano yake na Crown Media jana Desemba 5, 2024 ambapo alitoa ushauri kwa wasanii wa Tanzania kwa kuwataka kuwekeza zaidi kwenye Singeli kuliko Amapiano.
“Wivu mama wivuu hii ngoma ni powa, mimi nahisi Watanzania wangekuwa wameweka bidi kwa sound ya singeli kama vile waliweka bidi kwa amapiano muziki wa Tanzania ungekuwa umeenda mbali sana,”
“Singeli is a very uniqure sound na ni sound ambayo ni asili ya Tanzania, topic ambazo zinaimbwa kwenye ngoma za singeli zingine ni vichekesho zingine zinafundisha naiona tuu inaweza ikawa sound ambayo inaweza trend World Wide,” amesema Bien huku akiimba wimbo wa Wivu
Akizungumza kuhusu East Africa kukosa Grammy lakini anaamini kuwa muziki wa Singeli ukitiliwa maanani na kufanyiwa marekebisho kidogo basi huenda ukaleta tuzo hiyo kubwa ya muziki duniani.
“Singeli inaweza kuleta Grammy mbio sana singeli under Grammy ifanyie mixing, ifanyiwe mustering nzuri iandikwe vizuri katikati iwekwe tu mistari kidogo za kizungu kuwakilisha global, South Afrika wanaimba amapiano na watu hawaelewi lakini zinatembea,” amesema Bien
Mbali na hilo lakini pia ameweka wazi kuwa hivi karibuni naye anampango wa kujiunga katika muziki wa singeli.
Remix ya ‘Wivu’ ambayo Jay Combat amewashirikisha wasanii kama Dj Mushizo, Ibraah na Baddest 47 inaendelea kupenya ndani na nje ya nchi huku ikitizamwa zaidi ya mara milioni 2 katika mtandao wa YouTube.
Leave a Reply