Biden asema Trump aliiangusha Marekani wakati wa utawala wake

Biden asema Trump aliiangusha Marekani wakati wa utawala wake

Rais wa Marekani Joe Biden, leo amejibu Tangazo la rais wa zamani wa taifa hilo Donald Trump kwamba atawania kiti cha urais mwaka 2024, akisema chama cha Republican kiliiangusha Marekani alipokuwa madarakani.

Biden amesema Trump aliupora uchumi kwa manufaa ya matajiri, alishambulia huduma ya afya na haki za wanawake pamoja na kuchochea ghasia alipojaribu kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020 aliposhindwa.

Rais huyo wa zamani Donald Trump jana alizindua rasmi kampeni yake ya kuwania kiti cha urais kwa mara ya tatu katika wakati ambapo anakabiliwa na ukosoaji baada ya chama chake cha Republian kupata matokeo mabaya ya uchaguzi wa hivi karibuni.

Chanzo DW

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags