Rais wa marekani Joe Biden ameidhinisha kupelekwa kwa msaada wa dharura katika jimbo la New York kufuatia dhoruba kali ya theluji iliosababisha vifo vya zaidi ya 27 huku wengine maelfu wakiachwa bila nishati ya umeme.
Kikosi cha dharura cha uokoaji kimejitahidi kuokoa wakaazi walioathiriwa kutokana na kile mamalaka nchini humo imekiita dhoruba ya theluji ya karne ambayo imesababisha vifo vya zaidi ya watu 50 nchini Marekani na kutatiza mwenendo mzima wa usafiri hasa katika majimbo tisa.
Mamlaka katika jimbo la New York imeeleza hali kuwa mbaya zaidi hasa katika eneo la Buffalo huku miili ikigunduliwa kwenye magari, kingo za theluji na waokoaji wamekuwa wakikagua gari kwa gari wakitafuta waliofariki au walio hai.
Gavana wa New York Katheleen Hochul, amesema wanatazamia dhoruba itarejea tena ambapo barafu yenye urefu wa nchi 6 hadi 12 upande wa kusini wa Kaunti ya Erie na kusini kidogo mwa eneo hilo walipata theliji yenye urefu wa nchi 30 hadi 40 usiku wa kuamkia leo, hivyo ni mapema kutabiri kama ndio mwisho.
Aidha Gavana wa kaunti ya Erie ambapo hali mbaya zaidi ya hewa katika eneo hilo imeshuhudiwa Mark Poloncarz, amewaambia wanahabari kwamba idadi ya vifo imeongezeka kutokana na dhoruba hiyo ya theluji hadi vifo 12 kwa usiku wa kuamikia leo
"Ofisi ya idara ya afya Erie imethibitisha vifo 25 katika kaunti yote ya Erie, idadi hiyo inajumuishwa na ile ya mji wa Buffalo."
Alisema Mark na kuongeza kwamba wapo baadhi ambao wanaweza kupatikana Buffalo ambao idara ya afya haijawathibitisha wapo katika mchakato huo wa kuwathibitisha.
"kwa sasa hatuna taarifa kuhusu maeneo,jinsia au namana ya kifo, turatarajia kuwa na taarifa hizo hivi karibuni."
Inaelezwa kuwa Barabara nyingi ikiwemo zile zenye shughuli nyingi zilifungwa kutokana na kufunikwa kwa barafu.
Madereva wameonywa kutondesha magari yao barabarani pamoja na kwamba nchi ipo katika kipindi ambacho matumizi ya barabara yapo juu kutokana na watu wengi kusafiri.
Kikosi cha ulinzi cha taifa pamoja na timu zingine za uokoaji wameokoa mamia ya watu kutoka katika gari zilizofunikwa na theluji na nyumba ambazo hazina umeme, lakini mamalaka imesema kwamba watu zaidi huenda wamenasa kwenye theluji.
Karibu watu milioni 1.7 siku ya jumamosi walikosa huduma ya umeme huku wakipigwa na baridi kali. Idadi hiyo imepungua kwa kiasi kikubwa ingawaje bado kulikuwa na takriban wateja 50,000 wakiwa hawana huduma hiyo siku ya Jumatatu huko pwani ya mashariki mwa Marekani.
Leave a Reply