Biden aagiza mashirika ya ndege kuanza kulipa fidia

Biden aagiza mashirika ya ndege kuanza kulipa fidia

Rais wa Marekani, Joe Biden, ameagiza wizara ya uchukuzi kuandika kanuni mpya zitakazo yalazimu mashirika yote ya ndege kugharamia chakula na malazi ikiwa kwa uchelewaji au ughairishaji utakuwa ndani ya udhibiti wa shirika.

Ingawa baadhi ya sababu zitakazochangia kulipwa fidia ni pamoja na matatizo ya kiufundi na shirika kupungukiwa wafanyakazi huku fidia ikiwa ni pamoja na kupewa tiketi mpya hata kama abiria ataamua kutosafiri siku hiyo.

Hata hivyo endapo suala hilo litaanza utekelezaji, litawapa watumiaji wa usafiri wa anga ulinzi sawa na wasafiri waliopo katika umoja wa ulaya ambako mashirika hutakiwa kuwafidia abiria kwenye dharura za safari mbalimbali.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags