Biashara ya ufugaji cha sungura na faida yake

Biashara ya ufugaji cha sungura na faida yake

Na Habiba Mohamed

Niajeee niajeeeeeeee wasomaji wa Mwananchi Scoop. Kama kawa, kama dawa, kwenye kona yetu ya biashara tunakupa michongo ya kupata pesa kwa kukusanua na information za fursa za kibiashara. Ebwanaa kwenye biashara this week tunazungumzia biashara ya kilimo cha ufugaji wa sungura.

Alooooh! Wengi wetu tunafikiria kilimo ni hadi ushike jembe Ila katika kilimo cha ufugaji sungura imekuwa tofauti kidogo, ingawa watu wanachukulia poa ufugaji wa sungura. Aya twende pamoja kufahamu kwa undani biashara ya ufugaji wa sungura na faida yake.

Sungura ni mfugo anayezaliana kwa kasi kuliko baadhi ya mifugo mingine kwani huzaa kati ya watoto 5 hadi 14 kwa mara moja vilevile hubeba mimba kwa wastani wa mwezi mmoja, pia katika ufugaji wa sungura hauna gharama kubwa hivyo mtu yoyote aliyetayari kufanya shughuli ya ufugaji huu anaweza kumudu gharama.

Sungura akitunzwa katika mazingira mazuri mfano banda zuri linaloweza kubeba sungura bila kubanana na mikingio ya kutolea uchafu nje ie kinyesi na mikojo husaidia kuepukana na magonjwa ya ngozi na minyoo pia lishe yake ni rahisi kupatikana kama vile nyasi, mbogamboga kama vile sukumawiki, spinach, karoti vilevile mchanganyiko wa chakula (pellet) wenye vitamin na virutubisho na lishe bora kwa sungura.

NAMNA YA KUANZA UFUGAJI WA SUNGURA

Mtaji wa biashara hii hutegemea na mfugaji mwenyewe ataanza na sungura wa ngapi? Ila vitu vinavyohitajika ni;

Sungura matured/wazazi dume na jike ambapo sungura jike anabeba mimba kwa siku 28-32 na huzaa watoto 5-12. Sungura mmoja ni Tsh30,000

Kifaranga 2kg =18000/=

Cage (Banda) la vyumba 20 = 500,000/=

SOKO LA BIDHAA

-Sungura huuzwa kama kitoweo. Wataalamu wa afya wanasema nyama ya sungura ni nzuri kwani haina wingi wa mafuta ya choresto, ina wingi wa protein hivyo mtu yoyote anaweza kutumia hata wenye magonjwa ya kisukari na presha.

Licha ya kuuzwa kama kitoweo pia ngozi na mkojo wake huuzwa kwa matumizi mengine ya kutengeneza mapambo na mbolea, mkojo wa sungura hutumika kama kiwatilifu wadudu shambani.

Aidha nyama ya sungura hutumika mahotelini, supermarket na watu binafsi vilevile nyama ya sungura husafirishwa nje ya nchi.

FAIDA ZA UFUGAJI WA SUNGURA

  1. Kujipatia kitoweo (nyama,soseji)
  2. Kujiongezea kipato kwa kuuza, kwani 1kg ya nyama ya sungura ni Tsh9000 na sungura akiwa mzima huuzwa Tsh30000.
  3. Kujiajiri mwenyewe
  4. Kukuza uchumi wa nchi kwani nyama ya sungura husafirishwa hadi nje ya nchi.
  5. Hawana gharama katika kuwatunza kama wanyama wengine
  6. Sungura hutoa bidhaa aina nyingi mkojo, mbolea, nyama, ngozi.
  7. Linachukua eneo dogo katika ufugaji inategemea na aina ya banda kama la ndani au banda la nje.
  8. Kilimo endelevu. Sungura ana uwezo wa kuzaa mara kumi na mbili (12) kwa mwaka mmoja ila kitaalamu unashauriwa kumzalisha sungura mara sita (6) kwa mwaka Ili kusaidia awe na afya bora na kuzaa wototo wenye afya nzuri.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags