Biashara tatu zinazohitaji mtaji mdogo

Biashara tatu zinazohitaji mtaji mdogo

Kuna methali isemayo mdharau mwiba mguu huota tende msemo huu umesadiki katika baadhi ya biashara ambazo watu wengi wamekuwa wakizichukulia poa lakini ndiyo hizo hizo ambazo zimekuwa zikiwatoa kimasomaso baadhi ya wafanyabiashara.

Kupitia Biashara ya Mwananchi Scoop tunakudokeza wewe ambaye biashara rafiki ambazo unaweza kufanya na ukajipatia kipato

  • Biashara ya Mashuka na Duvert

Moja ya biashara ambayo watu wengi wanaiona kama haina faida ni hii ya mashuka na maduvert bila ya kufahamu kuwa imekuwa ikiwanufaisha wengi na kuwapatia faida.

Biashara ya maduvert nzuri zaidi kufanywa kwenye mikoa ambayo hali ya hewa ni baridi huku kwa upande wa mashuka yanauzika sehemu yoyote.

  • Biashara ya Nguo za Ndani

Zamani biashara hii ilikuwa ikiuzwa kwa usiri mkubwa  lakini kama tujuavyo maisha yanabadilika ambapo kwa sasa biashara ya kuuza nguo za ndani za kike/kiume imekuwa ikitangazwa hadi kwenye mitandao ya kijamii hiyo yote ni kutokana na kuwapatia wauzaji wake faida.

 

Hivyo basi unapofikiria kufanya biashara ukiwa na mtaji usiozidi laki moja nakushauri iangalie kwa kina biashara hii kwani ndiyo biashara ambayo unaweza kupata faida ya laki tano katika mtaji wa laki moja.

 Biashara ya Vipodozi

Najua mnajua lakini nawajuza zaidi, katika pitapita zako kwenye mitandao ya kijamii lazima ukutane na matangazo ya biashara ya vipodozi na urembo hivyo basi usikae nyumbani ukasema hauna kazi ya kufanya tafuta mtaji wako hata wa laki moja nenda kanunue vipodozi piga picha posti, watangazie wateja waone unachofanya  

Siku hizi hakuna kukaa na kubweteka kama unataka maokoto lazima upambane huku ukitumia fursa ya mitandao ya kijamii katika kujipatia wateja wapya kila siku

 

Mwisho wa yote unatakiwa kufahamu kuwa biashara inahitaji uvumilivu, kujitangaza, kujituma, lugha nzuri ni na kujiamini.

 

 

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post