Beyonce na Jay-Z washitakiwa

Beyonce na Jay-Z washitakiwa

Kundi la zamani la New Orleans limewashitaki wanamuziki Beyonce, Jay-Z na Big Freedia kwa ukiukwaji wa hakimiliki kutoka katika wimbo wa Beyonce wa ‘Break My Soul’ uliyotoka mwaka 2022.

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Usa today’ imeeleza kuwa kesi hiyo iliwasilishwa katika Shirikisho la Hakimiliki siku ya jana Jumatano Mei 22, 2024 katika wilaya ya Mashariki ya Louisiana, ambapo kundi hilo liliwahi kucheza ‘Showstoppaz’ linamshutumu Big Freedia kwa kutumia kinyume cha sheria maneno matatu katika wimbo wa ‘Explode’ 2014.

Katika kesi hiyo, washiriki wanne wa kundi hilo ambao ni Tessa Avie, Keva Bourgeois, Henri Braggs na Brian Clark , wanadai Big Freedia alichukua msemo kutoka kwenye wimbo wao wa mwaka 2002 uitwao ‘Release A Wiggle’.

Hivyo basi Beyonce ameingia katika kesi hiyo baada ya kuiga wimbo wa Big Freedia ‘Explode’ kwenye ngoma yake ya ‘Break My Soul’ iliyokuwepo kwenye albumu yake ya ‘Renaissance’ ya mwaka 2022.

Aidha siyo Beyonce tu na mumewe ambao wamehusishwa katika sakata hilo baadhi ya watu ambao wametajwa kuhusika ni pamoja na watayarishaji na kampuni zilizosambaza wimbo huo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags