Beyonce atimiza ndoto ya shabiki mwenye ulemavu, aliyekosa nafasi kwenye ndege

Beyonce atimiza ndoto ya shabiki mwenye ulemavu, aliyekosa nafasi kwenye ndege

Shabiki wa Beyonce mwenye ugonjwa wa kupooza hatimaye amefanikiwa kutimiza ndoto ya kumuona msanii huyo kwa mara ya kwanza baada ya kupata msaada wa 'tiketi' ya ndege na yakuingia kwenye show kutoka kwa Beyonce.

Shabiki huyo anafahamika kwa jina la Jon Hetherington ambaye anatumia wheelchair kutembelea kutokana na ulemavu aliyopata kwa ugonjwa wa kupooza, ametimiza ndoto yake, licha ya hapo awali kukata tamaa ya kumuona nyota huyo kutokana na kiti anacho tembelea.

Joh alieleza kuwa kila alipoenda kwenye usafiri wa ndege ili afike kwenye show ya Beyonce mashirika ya ndege ambayo hakuyataja majina yalimkatalia kusafiri na kiti chake kwani hakuna nafasi ya kutoshea kiti hicho ambacho kina kirefu wa inchi nne hivyo hawataweza kukipakia kwenye ndege.



Majibu hayo hayakumfurahisha Joh ndipo aliji-record video akilalamikia kilichotokea na kudai kuwa alingoja kwa miaka 25 ili aweze kufika kwenye show ya Beyonce lakini imeshindikana kutokana na kiti chake.

Hata hivyo video hiyo iliweza kumfikia Beyonce kuhusiana na kilichomkuta Joh, ndipo aliamua kutuma wawakilishi wake kumlipia Joh usafiri ambao ataweza kuingia yeye na kiti chake ili aweze kufika Arlington, Texas kwenye show.

Joh alifaniki kufika kwenye show na ameonesha shukrani zake za dhati kwa Beyonce na mama yake Ms Tina Knowles kwa kumtimizia ndoto yake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags