Mwanamuziki kutoka Marekani Beyonce amedaiwa kujitosa kufunika sakata la mumewe Jay Z hii ni baada ya Foundation ya BeyGOOD iliyopo chini ya msanii huyo kutoa fedha takribani dola 100,000 katika Chuo Kikuu cha sheria kilichopo Houston katika mji aliyozaliwa Beyonce.
Kulingana na Leonard Baynes, Mkuu wa Chuo cha Sheria Houston, ameweka wazi kuwa mchango wa dola 100,000 kutoka Foundation ya BeyGOOD utasaidia kufanikisha kuanzisha kliniki kamili ya haki ya jinai na kuboresha programu bora zaidi.
“Ninayo furaha kwamba Foundation ya BeyGOOD imetoa zawadi hii ya ukarimu kwa Chuo cha Sheria cha UH. Sio tu kwamba fedha hizi zitasaidia kuanzisha kliniki kamili ya haki ya jinai inayotoa huduma za kisheria bila malipo katika jamii yetu, bali pia zitaboresha zaidi programu zetu bora za sheria ya jinai na haki,” amesema Baynes.
Aidha kupitia mitandao ya kijamii wadau mbalimbali wametoa maoni kwa kudai kwamba Beyonce ameamua kujiongeza ili kufunika kesi inayomkabili mume wake Jay Z ya kutuhumiwa kumbaka mtoto wa miaka 13 tukio lililotokea mwaka 2000.
BeyGOOD ni shirika lililoanzishwa mwaka 2013 na mwanamuziki Beyonce kwa lengo la kusaidia jamii katika Nyanja mbalimbali kama vile Elimu, Afya, Haki pamoja na Biashara ndogo ndogo.
Leave a Reply