Bet yamuomba radhi Usher

Bet yamuomba radhi Usher

Waandaaji wa Tuzo za BET wamemuomba radhi mkali wa R&B Usher baada ya hotuba yake kutosikika kwa mashabiki walioko majumbani.

BETiliomba radhi kwa mshindi huyo mara nane wa Grammy siku ya jana Jumatatu Julai 1, ikieleza kuwa kutosikika kwa baadhi ya vipande vya hotuba hiyo kumetokana na matatizo ya kiufundi.

Aidha waandaaji hao walitoa shukrani zao kwa msanii huyo kwa kukubali kuhudhuria katika tukio hilo muhimu na kutoa hotuba fupi huku wakiwataalifui mashabiki ambao walikosa kusikia hotuba hiyo kuwa kwa sasa inapatikana katika majukwaa ya BET.

Utakumbuka Usher Raymond alishinda Tuzo ya BET 2024 katika kipengele cha Msanii Bora wa Kiume wa miondoko ya R&B kwa mara ya tano.

Tuzo hizo zilifanyika Jumapili Juni 30, katika Ukumbi wa Peacock Theater jijini Los Angeles huku Usher akiwapiku wasanii kama Chris Brown, Burna Boy, Drake, Fridayy, October London, Bryson Tiller na wengine.
.
.
.
#MwananScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags