Berlin yatangaza uwezo wa kupokea wakimbizi umefika kikomo

Berlin yatangaza uwezo wa kupokea wakimbizi umefika kikomo

Mji mkuu wa Ujerumani, Berlin umetangaza kuwa uwezo wake wa kupokea wakimbizi umefika kwenye ukomo. Seneta wa mji huo anayehusika na kuwaingiza wageni katika mji wao, Katja Kipping amesema kuwa hivi karibuni nafasi 6,000 za kuwapokea watu ziliundwa katika vituo vya kijumuiya na kufikisha idadi jumla ya nafasi 27,700. Licha ya ongezeko hilo, hivi sasa zinasalia nafasi 200 za kuwapokea watu.

Aidha, Kipping amesema idadi ya waomba hifadhi imeongezeka mjini humo mwaka huu, ikifika watu 12,237 katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka 2022, akiongeza kuwa wengi wao, ingawa sio wote, wataamua kubaki mjini Berlin.

Hata hivyo ukubwa wa tatizo umekithiri kutokana na maelfu ya wakimbizi kutoka Ukraine, ingawa mtiririko wao umepungua kwa kasi ikilinganishwa na siku za mwanzo za uvamizi wa Urusi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags