Ben: Kanumba angekuwa hai macho yote yangekuwa kwetu

Ben: Kanumba angekuwa hai macho yote yangekuwa kwetu

Mwigizaji Ben wakati akifanya mahojiano na @mwananchiscoop amesema kuwa kwa sasa kuna baadhi ya stori ambazo anafikiria kama angekuwepo Kanumba angezifanya vizuri zaidi kuliko zinavyofanywa na waigizaji wengine.

“Kuna stori ambazo huwa nawaza ningekuwa na ile ‘mashine’ yangu Kanumba basi kila mtu angeacha kuangalia kwingine angetutazama sisi tu, lakini ndiyo hivyo hayupo tena,” amesema

Hata hivyo mwigizaji huyu ameenda mbali zaidi na kuieleza mwananchi scoop kuwa enzi hizo walibahatika kucheza filamu na watu wa nje ya nchi, wamejifunza mambo makubwa na ndiyo maana kwa upande wake hapati tabu kwani hakuna kitu kigeni na ndiyo maana akipewa uhusika wowote anautendea haki.

“Sisi tuliobahatika kucheza na wasanii kutoka nchi nyingine tumebahatika kuwa na madini makubwa na ndiyo maana mimi ukiniweka popote nanyoosha kwa sababu hata robo hatujawafikia wasanii wa nje,” amesema Ben.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags