Baraka The Prince kurudi darasani, Amtaja Diarra wa Yanga

Baraka The Prince kurudi darasani, Amtaja Diarra wa Yanga

Ukifanya kazi nzuri inavuta wengine kujifunza je, unataka kuamini hilo, hiki ndicho alichokisema msanii wa #Bongofleva, Baraka the Prince, kuhusu kipa wa Yanga, #DjiguiDiarra anayemfurahisha jinsi anavyofanya kazi yake.

Msanii huyo ambaye ni shabiki wa ‘klabu’ ya  #Yanga, amesema Diarra akiwepo ‘golini’ anakuwa na amani kuona ‘timu’ inakuwa na ulinzi wa kutosha, hivyo kazi inabakia kwa washambuliaji kufunga.

"Diarra amekuja kuleta kitu tofauti, ambacho makipa wetu wazawa wanaweza wakajifunza kwa faida ya Taifa lao, anajiamini ana uwezo mzuri wa kutumia miguu, hivyo anawapunguzia kazi washambuliaji na kuwaongezea kujiamini,"amesema Baraka.

Kuhusu muziki Baraka amesema mwaka 2023 aliutumia kwa ajili ya kuandaa nyimbo za kutosha ambazo ataziachia mwaka huu.

"Nina nyimbo za kutosha, nilifanya hivyo kwa sababu mwaka huu (2024) narudi chuo kusoma Shahada ya Kwanza ya Uhandisi wa masuala ya simu (Tell Communication), kwani tayari nina Diploma nilioisoma 2013," amesema.

Mwimbaji huyo mwenye sauti nyororo na anayeimba nyimbo laini amebainisha kuwa anapenda nyimbo za Hiphop na baadhi ya wanamuziki anaowapenda ni kama Joh Makini, Fid Q na Nick Mbishi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags