Baraka The Prince alivyo mtolea nje Real Bexy kwenye ‘Kolabo’

Baraka The Prince alivyo mtolea nje Real Bexy kwenye ‘Kolabo’

Mwanamuziki chipukizi Real Bexy amefungukuka ambavyo Baraka The Prince alimtema kufanya naye ‘kolabo’ wakati anajitafuta kupenya kwenye game ya Bongo Fleva.

Akizungumza na moja ya chombo cha habari  amedai kuwa aliwahi kunyimwa ‘kolabo’ na Baraka licha ya  kuwahi kuwa marafiki na kumwambia akue kwanza kimuziki ndiyo amuombe ‘kolabo’.

Aidha ameeleza kuwa alivyotoa wimbo wake wa kwanza kipindi ambacho Baraka havumi, alimfata na kumsifia huku akidai kuwa yupo tayari kufanya naye kazi.

Hata hivyo Real Bexy amedai kuwa baada ya Baraka kumfata ilibidi na yeye amvimbie, kama alivyofanyiwa mwanzo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post