Bango laangukia mashabiki uwanjani

Bango laangukia mashabiki uwanjani

Mashabiki wasiopungua 20, wanadaiwa kuumia vibaya baada ya kuangukiwa na bango wakati mchezo dhidi ya klabu ya #Stevo na #FCTwente huko nchini Uholanzi.

Taarifa zinaeleza kuwa tukio lilitokea nyuma ya ‘goli’ wakati mchezo wa kirafiki wa Twete na Stevo unaendelea hali iliyozua taharuki na kusababisha hadi Helkopta za uokoaji kuwasili ili kutoa msaada.

Baada ya tukio hilo mwamuzi alisimamisha mchezo huo ambao baadae uliahirishwa na baadhi ya wachezaji walisogea eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada.

Hata hivyo kabla ya mchezo kulikuwa na fataki zilizotoa moshi mwekundu ambazo ziliwashwa na mashabiki na baada ya tukio hilo, moshi huo ulisababisha kuwepo na ugumu zaidi katika uokoaji.

Ingawa taarifa kutoka tovuti ya Oost zimeeleza kuwa hakuna aliyefariki katika majeruhi waliookolewa na klabu ya FC Twente pia imetoa taarifa kuwa wapo karibu na mashabiki zao waliopata madhara ambao kwa sasa wanaendelea vizuri kiafya.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags