Baking cakes using a gas stove

Baking cakes using a gas stove

Mambo vipi! Uko zako chuoni unapasua kichwa ni biashara gani ya kufanya fastafasta ambayo haitakugharimu saana!  Leo kwenye nipe dili nakusogezea mchongo huu hapa, wala usichanganyikiwe, just relax hujachelewa! Tumia fursa hii hapa, hata ukiwa zako hostel una uwezo wa kupiga hela kwa kutumia akili ndogo tu.

Chukua hii, jifunze nami namna gani utaweza kupika keki kwa kutumia jiko la gesi.

Mahitaji muhimu

ü Maziwa nusu kikombe

ü Siagi robo

ü Unga wa ngano robo

ü Sukari robo

ü Vanilla kijiko 1 kikubwa (cha chakula)

ü Baking powder kijiko 1 kikubwa

ü Bila kusahau kwenye upishi wenyewe sasa zingatia uwepo wa jiko la Gesi 

ü Mchanga au chumvi

 

Namna ya kupika keki

Tunaanzia hapa, chukua blueband robo yenye ujazo wa gramu 250, sukari nusu kikopo, maziwa nusu kikombe.

Baada ya hapo utasaga sukari yako hadi ifike hatua ya kuwa unga unga, unga robo kilo unahitaji mayai matatu, kisha changanya sukari na mayai, hadi utakapoona mchanganyiko huo unatoa povu, weka vanilla kifuniko kimoja.

Halafu weka unga wako wa ngano kwa kipimo kilekile ukitumia kikopo cha blueband, jaza unga hadi juu kisha baking poda kijiko kimoja kikubwa.

 

  • MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA KUPIKA KEKI YAKO

Hakikisha ukiwa unatumia jiko la gesi kwanza weka sufuria yako jikoni, kisha pakaza mchanga chini ya hiyo sufuria au chumvi ili kuzuia moto mwingi kupita na utawasha jiko lako ukiwa umeweka moto wa saizi.

 

Chukua sufuria yako ambayo umeiandaa kwa ajili ya kupikia keki ambapo utaipaka mafuta kwa ndani kisha utaiwekea unga kidogo kwa kupaka kwenye sufuria ambayo umeiandaa kwa ajili ya kupikia keki yako.

 

Unga huo utasaidia kuzuia keki kuganda kwenye sufuria wakati ikiwa tayari.

Kisha unaweza kutumia dk 40 hadi 45. Jitahidi kuwe na moto wa saizi ya kati ili keki yako itoke vizuri bila kuungua.

Eebwana eeeeh! Leo nimekupa dili hilo. Kwa shilingi elfu 10000 tu unaweza kutengeneza keki yako! sasa kazi kwako kuingia mzigoni, hakikisha unafuata maelekezo twenzetu tukasake manoti.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags