Bahati Kenya alia na Genius Jini x66 kufuta wimbo wake mpya

Bahati Kenya alia na Genius Jini x66 kufuta wimbo wake mpya

Msanii kutoka nchini Kenya, Bahati kupitia Instagram yake ame-share screenshoot kutoka katika mtandao wa YouTube ikionesha kuwa wimbo wake mpya wa 'Huyu' kuwa umefutwa kwa sababu ame-copy kutoka kwa mzalishaji wa muziki na msanii wa Bongo Fleva , Genius X66.

Bahati amemlaumu Genius Jini X66 kwa kumfutia wimbo wake uliyokuwa umefika trending number 2, huku akiuliza kuwa msanii huyo ni nani mbona hamfahamu?.

Kwa upande wa Genius naye hajaacha lipite na kuamua kujibu mapigo na kueleza kuwa Bahati amedai hamfahamu lakini taratibu atamjua yeye ni nani.

Hata hivyo inaonesha siku sita zilizopita Genius Jini X66 alitumia ujumbe kwa Bahati kuhusiana na tuhuma hizo za ku-copy wimbo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post