Babu Tale afunguka ishu ya Diamond kuhusishwa na Diddy

Babu Tale afunguka ishu ya Diamond kuhusishwa na Diddy

Kufuatia tuhuma zinazomkabili mkali wa Hip hop kutoka Marekani Diddy, Sean ‘Diddy’ Comb huku baadhi ya mastaa mbalimbali kuhusishwa kwenye kesi zake, meneja wa msanii wa Bongo Fleva, Diamond, Babu Tale amefunguka yaliyotokea baada ya kutembelea nyumbani kwa staa huyo.

Akizungumza na Rick Media, Babu Tale amesema walikwenda nyumbani kwa Diddy na waliitwa chumbani kwake kwenda kuangalia filamu lakini mtayarishaji wa muziki kutoka Marekani (aliyekuwa mwenyeji wao) Swizz Beatz alikataa wasiende.

“Sisi tulienda kama tulivyotoa taarifa hapo awali na tulitoka salama, jana ndiyo nimejua kwamba Swizz Beatz alikuwa akitulinda kinoma, kwanza tulipofika tulikaa nje.

"Diddy akatangulia chumbani juu anaangalia movie wafanyakazi wake wawili wakaja kutuchukua kwenda kula, baada ya muda akawatuma twende chumbani kwa Diddy tukaangalie movie lakini Swizz akawa mkali na tukaondoka bila kuaga kwahiyo sisi tukawa tunajua kuwa brother (Swizz Beatz) ametubania, kumbe alikuwa anatulinda,” amesema Babu Tale

Babu Tale ametoa ufafanuzi huo baada ya minong’ono kusambaa kuhusu safari yao nyumbani kwa Diddy, baada ya kipande cha video kikimuonyesha Diamond akifanyiwa mahojiano akisema kuwa baadhi ya mambo yaliyofanyika nyumbani kwa staa huyo sio ya kuwekwa kwenye vyombo vya habari.

“Ni kweli tulienda kwa Diddy nafikiri ilikuwa siku moja kabla ya uhuru wa Marekani, tulienda kwa Diddy usiku tukakaa kuna vitu tukafanya sema yaliyofanyika yalikuwa siyo ya kuposti kwa sababu yana mambo yajayo mbele,” alisema Diamond kwenye moja ya mahojiano yake aliyofanya miaka mitatu iliyopita.

Kwa sasa Diddy amezuiliwa katika gereza la ‘The Metropolitan Detention Center (MDC) kwa tuhuma za ulaghai wa kingono na usafirishaji wa binadamu ili kujihusisha na biashara hiyo ya ngono, huku zaidi ya chupa 1,000 za mafuta na vilainishi vikikutwa katika nyumba yake ya Miami na New York






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags