Baada ya kutoka jela Young Thug aanza na hili

Baada ya kutoka jela Young Thug aanza na hili

Ikiwa imepita wiki moja tangu rapa kutoka jijini Atlanta Marekani, Young Thug kutoka gerezani kutokana na makosa yaliokuwa yakimkabili, hatimaye ameanza kutekeleza adhabu alizopewa huku akitumikia kifungo cha nje

Utakumbuka kuwa adhabu alizopewa Thug baada ya kutoka gerezani ni kujishughulisha na kazi mbalimbali za kijamii na kutumia Sanaa yake kama sehemu ya kuelimisha, huku akipunguziwa idadi ya watu wa kuwasiliano nao na kutojihusisha na magenge ya wahuni wala kuimba kwa kushawishi ugomvi baina ya magenge ya wahuni.

Ikiwa ni moja ya kutumikia kifungo chake cha nje Thug, baada ya kutoka Gerezani aliweza kuwasiliana kwa njia ya simu na wanafunzi wa shule anayofundishia mwanasheria wake aitwaye Brian Steel kwa kuwaasa wanafunzi kuwa na tabia nzuri na kuzingatia masomo yao ili watatue changamoto za watu wengine.

Thug alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya kuendesha magenge ya wahuni, ulanguzi wa dawa za kulevya na utakatishaji fedha. Alitoka gerezaji Octoba 31, mwaka huu kwa masharti ikiwemo kifungo cha nje kwa miaka mitatu huku akiwa amefungwa kifaa maalumu mguuni (Ankle Monitor) kwa ajili ya kufuatilia nyendo zake.

Hata hivyo baada ya kumalizika kifungo hicho atatumikia miaka 15 chini ya uangalizi maalumu pamoja na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii huku akipewa angalizo kwani anaweza kutumikia kifungo cha miaka 20 jela endapo atakiuka sharti lolote alilopewa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags