Baada ya kushindwa kupiga kura, Rihanna akimbilia kwao

Baada ya kushindwa kupiga kura, Rihanna akimbilia kwao

Baada ya mwanamuziki kutoka katika visiwa vya Barbados, Rihanna kushindwa kushiriki katika zoezi la kupiga kura kumchagua rais wa Marekani, sasa ameamua kutimkia katika mji aliyozaliwa.

Kufuatia na video inayoendelea kusambaa kupitia mitandao ya kijamii Riri ameonekana akIfurahia wakati wake katika visiwa vya kwao ambapo alifika katika mji huo aliyozaliwa kwa ajili ya kuzindua bidhaa zake za ‘Fenty Beauty’.

Rihanna hakuruhusiwa kupiga kura kumchagua raisi anayemtaka nchini humo kutokana na kutokuwa na Uraia wa nchi hiyo, ambapo siku moja kabla ya kupiga kura alitania kuwa anatamani kuingia katika sehemu za kupiga kura na kitambulisho na mwanaye.

“Mimi nikijaribu kuingia kwenye kituo cha kupiga kura kwa kutumia pasipoti ya mwanangu”, aliandika Riri huku akiwasisitiza mashabiki zake kupiga kura kwa kiongozi wanaye mtaka.

Rihanna alihamia Marekani mwaka 2005 akitokea katika visiwa vya Barbados ambapo alifika nchini humo kwa ajili ya biashara zake za muziki, lakini mwaka 2021 alinunua nyumba ya kuishi nchini humo katika mji wa Hollywood Hills.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags