Mchezaji wa klabu ya Yanga Stephane Aziz Ki ameshare zawadi aliyopatiwa na rafiki yake mwigizaji na mfanyabiashara Hamisa Mobetto.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa mchezaji huyo ameshare zawadi ya viatu ambavyo ni mahususi kwa ajili ya kuchezea mpira wa miguu huku akitoa shukrani kwa kuandika ‘Asante Boss”.
Wawili hao wamekuwa kwenye ukaribu kwa muda mrefu huku baadhi ya wadau wakiwahusisha kuwa kwenye mahusiano licha ya Mobetto kukataa kuwa yeye namchezaji huyo hawana uhusiano wowote.
Utakumbuka kuwa Mobetto kwenye moja ya mahojiano yake aliweka wazi kuwa hana uhusiano na kigogo yeyote wa soka na pia wala Azizi Ki si mpenziwe kama baadhi ya watu wanavyodhani, akisisitiza nyota huyo wa boli ni rafiki yake na anamshabikia japo yeye ni shabiki wa Simba
Leave a Reply