Aziz Ki hana mpango wa kuondoka Yanga

Aziz Ki hana mpango wa kuondoka Yanga

Baada ya Yanga kutolewa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Mamelodi Sundowns kwa mikwaju ya penalti hatua ya robo fainali, kiungo mshambuliaji wa ‘timu’ hiyo, Stephane Aziz KI ameandika katika ukurasa wake wa Instagram ujumbe wa kumshukuru Rais Samia pamoja na mashabiki kwa kuwa nao pamoja kwenye safari ya michuano hiyo msimu huu 2023/2024.

Katika ujumbe huo upande wa ‘komenti’ KI amemjibu shabiki aliyeandika kuhusu yeye kuondoka ‘klabuni’ hapo msimu ujao kutokana na kufanya vizuri kwenye mashindano na ‘klabu’ nyingi kutaka huduma yake.

Ameandika; “Huna baya mwamba sana, najua msimu ujao utaondoka maana naona Mamelodi wanataka kukusajili, najua utaondoka.”

KI amejibu; “Sina matarajio ya kuondoka Yanga kwa sasa kwani sijafanikisha malengo yaliyonileta hapa, bado klabu hii ninayoipenda kwa moyo wangu wote inanidai, hata pesa haitaweza kujaza upendo nilionao kwa ‘klabu’ hii, lala kwa amani shabiki bado sijamaliza dhamira yangu.”

Ikumbukwe KI amebakiza miezi minne kumaliza mkataba wake na Yanga ambao alisaini msimu wa 2022\2023.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags