Aziz ki, Chama wafungiwa mechi tatu

Aziz ki, Chama wafungiwa mechi tatu

 

Kamati ya usimamizi na uendeshaji ya bodi ya Ligi Kuu (TPLB) leo imetoa adhabu kwa wachezaji wa Simba na Yanga kwa kuvunja kanuni.

Staa wa Yanga Stephan Aziz Ki na Staa wa Simba SC Clatous Chota Chama wamefungiwa mechi tatu kila mmoja na faini ya Tsh laki tano (500,000) kwa kosa la kushindwa kufuata kanuni za mchezo.



Chama na Azizi Ki wote kwa pamoja wakati wa mchezo wa Simba na Yanga uliochezwa October 23 2022 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya 1-1 hawakusalimiana na Wachezaju wa Timu pinzani kwa kile kilochodaiwa kutegeana kuingia uwanjani hadi tukio la kusalimiana lilipopita.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags