Azikwa hai kwa siku 7 akitengeneza kontenti ya youtube

Azikwa hai kwa siku 7 akitengeneza kontenti ya youtube

Mwanaume mmoja kutoka nchini Marekani ambaye pia ni mwandishi wa habari wa mitandaoni anayefahamika kwa jina la Jimmy Donaldson maarufu kama Mr Beast ame-trend kupitia mitandao ya kijamii baada ya kujirekodi akiwa amezikwa hai katika jeneza la kioo ndani ya kaburi la futi sita kwa muda wa siku saba.

Tukio hilo lilirushwa mubashara katika ukurasa wake wa YouTube ambao una wafuasi milioni 212 na video hiyo akiwa kaburini imefikisha jumla ya watazamaji milioni 63 ikiwa ni siku mbili zipite tangu akiwa ameiachia rasmi.


Katika kaburi hilo kulikuwa na maji, sehemu ya kujisaidia na eneo ambalo linatoa na kuingiza hewa na kuweka kamera kila kona kwa nia ya kuangalia kila kitu kama mambo yataenda vibaya.

Licha ya kukaa siku saba katika kaburi hilo alionekana kuanza kupatwa na tatizo la kisaikolojia kufuatiwa na kulia mara kwa mara baada ya kuwa na hofu ya kuwa huwenda asisimame tena na kuganda kwa damu kwenye miguu kutokana na kulala muda mrefu.

Hii si mara ya kwanza kwa Mr Beast kufukiwa kaburini akiwa hai mwaka 2021 alizikwa akiwa hai kwa masaa 50, hivyo basi amevunja rekodi yake ya mwaka huo baada ya kuzikwa kwa siku saba.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags