Azaboi na ndoto ya kubadilisha maisha ya vijana wachekeshaji

Azaboi na ndoto ya kubadilisha maisha ya vijana wachekeshaji

Heeeeey!!sasa tuwekane sawa sasa hii ni weekend nyengine bhana I hope mko sawa wenetu wanguvu hatuna budi kukusogezea kipengele cha burudani na michezo ambapo utapata kuyajua maisha ya wasanii, wachekeshaji na wanasoka kwa undani Zaidi.

Leo nakukutanisha nakijana mpambanaji anaepambania ndoto zake na za vijana wengine najua mnamfahamu lakini leo utapata kumjua kwa undani Zaidi Azaboi.

Mwamba huyu jina lake ambalo liko katika kitambulisho cha taifa ni Issac Feliza lakini lakutafutia ugali bwana ni Azaboi kama unavyoelewa ni kijana mchekeshaji ambae anatokea katika kundi maarufu la uchekeshaji ‘Cheka tuu’.

Ukizungumzia Issac au Azaboy ni mtu wa aina gani amefunguka na kueleza kuwa “ Yaani huwezi kutaja viumbe wavumilivu Duniani usinitaje kutokana na  hustles zangu mimi ni mtu ambae napenda sana mafanikio na kuwafanikisha vijana wenzangu kufikia wanapo pataka, ni mtu amabae nina upendo na wengine na nimvumilivu pia” amesema Issac

Safari yake ya upambanaji katika tasnia yake ya uchekeshaji imeanza mbali kidogo enzi akiwa shule huko jijini Dodoma alijikita na uimbaji kwenye sherehe mashuleni, lakini fani ya uchekeshaji ilikuja tuu baada ya alichokuwaa akikiimba kuwa furahisha watu.

“Nilikuwa sitaki kupitwa na kitu chochote nikiwa shuleni  nilipo fika chuo nikaanza standa up comedy baada ya kuhitimu masomo yangu ya elimu ya juu ndipo nikapata nafasi ya kujiunga na jukwaa la cheka tu comedy search” amesema Azaboi

Naam kama unavyojua safari ya mafanikio inamisukosuko mingi sana nakueleza kuwa kwa upande wake changamoto hazitoshi kuelezea kwa maneno machache maana ninyingi lakini anakiri Mungu ni mkubwa yeye anaendelea na safari yake ya upambanaji.

Katika kufanya kazi lazima mtu upende unacho kifanya kwa mwamba huyu mambo yanayo mfuraisha katika harakati zake hizo nimengi ila kubwa ni maendeleao mazuri  amabayo Mungu anayoyaruhusu katika tasnia yake kuwa mbunifu katika kazi yake.

Anaendelea kusema hajawahi kujibana kwenye kufanya uchekeshaji maana ana vutiwa na watu wengi sana hususani marafiki zake wanao mzunguka kwa kumapa sifa ya kile anacho kifanya lakini anavutiwa zaidi na comedians smart.

“Nina mengi ambayo hata  mimi siwezi kuyatabiri ila cha uhakika ni contents nyingi na ubunifu ilinizidi kuwa mzuri katika tasinia yangu   hichi kitu kinanifanya nijivunie sana mimi” amesema Azaboi

Jambo amabalo hatokuja kulisahau ni kukumbuka pesa yake ya kwanza kuimiliki katika talanta yake ya uchekeshaji ambayo ilikuwa ni shilingi laki nne aliitumia kwa kununulia kitanda kikubwa kuliko geto lake hahahahahhaa!!! Si unajua tena ile panic ya kushika pesa ambayo umeitolea jasho kwa mara ya kwanza.

Kuhusiana na nani amechagiza mafanikio yake mpaka sasa, hakutaka kuwa mchoyo wa fadhira “Msimamizi wetu au niseme tajiri ambae ndio sababu ya cheka tu Coy Mzungu nahisi kama ameshushwa na Mungu kutusaidia sisi vijana kutimiza malengo yetu yeye ndo aliefanya mpaka mimi nifike hapa” Amesema Azaboi

Kwa upande wa role model wake ni nani bwana mwamba huyu kaamua kukacha na kueleza kuwa hajawahi kujibana sana katika jambo hilo maana anavutiwa na watu wengi sana hususani marafiki wanaomzunguka vile vile na wale comedians smart.

Vijana wengi wamekuwa wakiishi na talanta zao bila kufanyiwa kazi ila kwa kuwa yeye walau amefika mahali furani katika mafanikio na anaendelea kupasua miamba basi atafanya kitu kwa vijana wengine ambao wapo tu mtaani na wanatamani kuwa wachekeshaji kama yeye.

Siku zote kila mwanadamu anandoto za kuzifikia, katika kufanya kazi kwa muda mrefu kwa upande wa mchekeshaji huyu yeye alifunguka na kueleza kuwa “Kwa upande wangu mimi nina ndoto za kufanya makubwa sana ambayo yataipunguzia Serikali mzigo kwa kutengeneza ajira nyingi yaani kuwa chanzo cha watu kunifaika na kuongeza pato kwa Taifa” amesema Azaboi

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags