Aweka rekodi ya kupiga push-up 1,575 ndani ya saa moja

Aweka rekodi ya kupiga push-up 1,575 ndani ya saa moja

Mwanamke mmoja kutoka Canada mwenye umri wa miaka 60 aitwaye DonnaJean Wilde, ameweka rekodi ya dunia kwa kupiga push-up nyingi zaidi ndani ya saa moja.

Kwa mujibu wa kitabu cha rekodi ya dunia ‘Guinness World Records’ mwanamke huyo mwenye wajukuu 12 jina lake liliingia katika kitabu hicho kwa kupiga push-up 1,575 kwa dakika 60.

Aidha kwa mujibu ya mwanamama huyo alieleza kuwa alilifanikisha hilo kutokana na mazoezi aliyokuwa akiyafanya ambapo alikuwa akipiga push-up 500 kila siku asubuhi.

Hii si mara ya kwanza kwa Wilde kushinda kwani mapema mwaka huu aliweka rekodi ya dunia kwa wanawake kwenye planking, akishikilia nafasi hiyo kwa saa 4.5.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags