Avunja rekodi ya kuishi chini ya maji siku 75

Avunja rekodi ya kuishi chini ya maji siku 75

Mtafiti mmoja aliefahamika kwa jina la Joseph Dituri kutoka nchini Marekani amevunja rekodi ya dunia baada ya kuishi chini ya maji Zaidi ya siku 75 chini ya rasi ya 30ft-deep huko Key Largo, Florida.

Mtafiti huyo ameeleza kuwa hana mpango wa kuacha bado angekaa hapo kwa angalau siku 100.

"Lengo langu tangu siku ya kwanza limekuwa kuhamasisha vizazi vijavyo, kuwahoji wanasayansi wanaosoma maisha chini ya bahari na kujifunza jinsi mwili wa binadamu unavyofanya kazi katika mazingira magumu," amesema Dituri

Ikumbukwe tu rekodi ya awali ya dunia ya siku nyingi za kuishi chini ya maji kwa presha ya mazingira 73 ilianzishwa na maprofesa wawili mnamo mwaka 2014 katika eneo sawa na Key Largo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post