Avunja rekodi kwa kuwa na pembe nyingi kichwani

Avunja rekodi kwa kuwa na pembe nyingi kichwani

Mwanaume mmoja kutoka pwani ya Praia Grande karibu na São Paulo nchini #Brazili, Michel 'Diabao' Praddo (47) maarufu kama ‘Shetani wa Kibinadamu’ amevunja rekodi ya dunia ya Guinness kwa kuwa na idadi nyingi ya pembe kichwani.

#Diabao anadaiwa kupandikiza pembe 33 kichwani kwake kama sehemu ya jitihada za kubadilisha sura yake kabisa.

Kufuatiwa na moja ya mahojiano yake alieleza kuwa ilikuwa ni ndoto yake kuingia katika kitabu cha Guinness huku akimshinda Milan kutoka Italia mwenye pembe 18.

Aidha mwaka jana, #Diabao alifanyiwa upasuaji wa kuondoa kidole cha kati na kupandikizwa pembe mdomoni mwake, ambayo anasema iligharimu £790.

Asilimia 80 ya mwili wake umechorwa kwa #tattoo huku baadhi ya viungo vyake kuviondoa ikiwemo, #Masikio, Kukata ncha ya pua , kidole cha pete mkono wa kushoto, chuchu na vinginevyo.
.
.
#mwananchiscoop
#burudikanasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post