Auza mtoto wa siku tano akatengeneze pua

Auza mtoto wa siku tano akatengeneze pua

Hii sasa balaa aiseee, dunia simama nishuke  ukistaajabu ya Mussa, utayaona ya Firauni. Mwanamke mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa amekamatwa na kushtakiwa baada ya kukutwa akimuuza mwanaye wa kiume wa kumzaa, mwenye umri wa siku tano, huko Dagestan, jiji la Kaspiysk, Kusini mwa Urusi.

Mwanamke  huyo mwenye plasta (33) amesema alitaka kumuuza mwanaye huyo ili apate pesa za kwenda kufanya surgery ya kurekebisha pua yake hiyo ili azidi kuwa mzuri zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari na polisi nchini humo  mrembo huyo baada ya kuzaa alimwambia rafiki yake hana nia ya kulea mtoto mchanga.

Sambamba na hayo tayari wanashtakiwa kwa makosa kwa biashara hiyo haramu ya kuuziana watu.

Hata hivyo  mama  huyo alishazungumza na mwanamke na mwanaume yaani (couple) waliokuwa wameshatoa fedha kiasi ili kumnunua mtoto husika ambapo jumla walikubaliana manunuzi hayo yawe £2900 ambazo sio chini ya milioni 7.9 za Tanzania lakini walimpa asilimia 10 tu ya malipo yote (£274).

Wapenzi waliotaka kununua mtoto huyo aliyezaliwa Aprili 25, 2022, wakati wakihojiwa na polisi wamesema, awali mwanamke  huyo pichani aliwaambia hana kazi wala sehemu ya kuishi ndio anahitaji pesa.

Baada ya kuwapa mtoto, aliugua wakampeleka Caspian City Central Hospital, walipofika walihojiwa cheti cha mtoto lakini hawakuwa nacho, waliporudi kwa huyo mama halisi wa mtoto kumuuliza kuhusu cheti cha mtoto akawataka wamalizie malipo yaliyobaki ndipo awape cheti.

Baada ya kupokea pesa hizo Mei 26, 2022, mama aliwawaambia pesa hizo za kumuuza mwanae amepanga akafanye surgery ya pua ili kuongeza ubora wa urembo wake. Lakini pia hana kazi wala mahali pa kuishi, hivyo zitamsaidia katika maisha yake.

Na kabla hawajamalizana kulipana malipo ndio wote watatu wakadakwa na vyombo vya sheria kwa biashara hiyo haramu ya kuuziana watu.

Aiseee hii sasa hatari dondosha comment yako hapo chini kuhusiana na mkasa huu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post