Aucho afungiwa mechi tatu

Aucho afungiwa mechi tatu

Nyota wa Yanga, Khalid Aucho aamefungiwa kutocheza michezo mitatu na faini ya Sh500, 000 (laki tano) katika mchezo dhidi ya Coastal Union Novemba 8 katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Kufungiwa nyota huyo ni kutokana na kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Ibrahim Ajibu wa Coastal Union.

Katika mchezo huo pia Coastal Union imetozwa Sh1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la wachezaji kuchelewa kutoka nje ya chumba cha kuvalia nguo, jambo lililosababisha mchezo kuchelewa kuanza kupindi cha kwanza na baada ya mapumziko, hivyo kuharibu program za mrusha matangazo ya runinga (Azam TV) ambaye ni mdhamini mwenye haki za matangazo ya runinga

Aucho atakosa mechi ya Mtibwa Sugar Disemba 16, Tabora United Disemba 22 na 26 dhidi ya Kagera Sugar.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags